EDEN QUICK PIG BOOST ni kirutubisho maalumu kilichoundwa kwa ajili ya nguruwe wa aina zote ili kuwapatia madini na virutubisho muhimu vinavyosaidia ukuaji bora, afya imara na kuongeza ufanisi wa uzalishaji. Kirutubisho hiki kina mchanganyiko kamili wa madini muhimu kama Calcium, Phosphorus, Iron, Copper, Manganese, Zinc, Iodine pamoja na virutubisho vingine vinavyoimarisha mwili wa nguruwe na kuboresha mmeng’enyo wa chakula.
Kwa kutumia Pig Boost, wafugaji hupata uhakika wa lishe iliyokamilika inayoongeza kasi ya ukuaji, kuimarisha mifupa, kuongeza hamu ya kula na kupunguza magonjwa yatokanayo na upungufu wa madini.

